Vitabu Nilivyosoma Mwaka 2019

Fadhy Mtanga
5 min readDec 28, 2019

--

MWAKA 2019 upo ukingoni kabisa. Kama ilivyo ada, miongoni mwa jamii za wasoma vitabu, nami ninatoa orodha ya vitabu nilivyovisoma kwa mwaka mzima. Kipindi kama hiki mwaka jana niliweka kusudio la kusoma vitabu 50. Nilipunguza malengo kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza, nilikuwa masomoni. Hivyo, robo tatu yote ya 2019 ilinikuta nikikimbizana na assignments, tests na mitihani. Sababu ya pili, nilitaka kuandika zaidi.

Leo hii, nakuleteeni orodha ya vitabu nilivyovisoma. Nimevigawa kwa makundi. Hata hivyo, sitoweka vitabu vyangu, kwa kuwa ni utaratibu wangu kurudia kuvisoma kila nipatapo wasaa.

RIWAYA ZA KISWAHILI

Hisani huanzia nyumbani, siku zote. Kiswahili ni lugha tamu. Hivyo, hata vitabu vinavyoandikwa kwa Kiswahili ni miongoni mwa vitabu vinavyoleta ladha katika usomaji wake. Mwaka huu nimesoma vitabu vifuatavyo katika Kiswahili:

  1. Kiroba Cheusi — Laura Pettie (kama mhariri)

2. Sayantisti — Issa Abrahams (kama mhariri)

3. Daladala Kutoka Mbagala — Mussa M. Shekinyashi (kama mhariri)

4. Nenda, Ila Usiende Na Hisia Zangu — Hassan Mboneche (kama mhariri)

5. Kivuli — A. E. Musiba

6. Mdhamini — Japhet Nyang’oro Sudi

7. Patapotea — Japhet Nyang’oro Sudi

8. Ufukwe wa Madagascar — Kevin Mponda

9. Kosa Langu Nini — Dalton Asukile

10. Kijiji Kisicho na Makaburi — Dickson Mtalaze

11. Mtutu wa Bunduki — Kevin Mponda

RIWAYA ZA KINGEREZA

Waandishi Sidney Sheldon, James Hadley Chase, John Grisham na Mario Puzo huwarudia kuwasoma mara kwa mara. Ni wazi, uandishi wangu umeathiriwa kwa kiasi kikubwa na Sidney. Ili nizidi kuwa mwanafunzi wake, yanipasa kumsoma mara kwa mara. Ukiacha waandishi hao wanne, pia nimewasoma waandishi wengine.

12. Hearts Among Ourselves — Assumpta Happy Umwagarwa

13. Sands of Time — Sidney Sheldon

14. The Rage of Angels — Sidney Sheldon

15. The Witness To A Trial — John Grisham

16. The Whistler — John Grisham

17. The Street Lawyer — John Grisham

18. The Godfather — Mario Puzo

19. The Sicilian — Mario Puzo

20. The Break — Marian Keyes

21. Mission to Venice — James Hadley Chase

22. Why Pick on Me — James Hadley Chase

23. You Find Him — I’ll Fix Him — James Hadley Chase

24. The Double Shuffle — James Hadley Chase

25. The Black Prism — Brent Weeks

26. Beyond the Shadows — Brent Weeks

27. The Winter Stands Alone — Paulo Coelho

WASIFU NA TAWASIFU

Mwaka huu, niliamua kuongeza idadi ya wasifu na tawasifu. Kuna mengi sana ya kujifunza kupitia masimulizi ya maisha ya watu wengine.

28. Truth, Lies and Alibis: A Winnie Mandela Story — Fred Bridgland

29. The Leading — Sir Alex Ferguson & Michael Moritz

30. Kikwete: Safari ya Ikulu — Ben R. Mtobwa

31. Born A Crime — Trevor Noah

32. Jay — Z: A Biography of Hiphop Icon — Jeff Burlingame

33. Trevor Noah: Biography of the Famous South African Comedian — Lawrence Barnes

34. Robben Island Hell-Hole: Reminiscence of a Political Prisoner — Moses Dlamini

35. The Man Who Founded the ANC: A Biography of Pixley ka Isaka Seme — Bongani Ngoulunga

36. Bob Marley: A Biography — David V. Moskowitz

37. My Life with Bob Marley: No Woman No Cry — Rita Marley

VITABU KUHUSU RWANDA

Nilipomaliza kukisoma kitabu cha Hearts Among Ourselves, nilijikuta ninahitaji kusoma vitabu zaidi kuhusiana na Rwanda. Nilihitaji kujifunza kwa kina juu ya sababu za kihistoria, kisiasa na kijamii zilizopelekea janga kubwa kama lile la mauaji ya kimbari. Kulikuwa na viashiria gani vilivyopuuzwa? Wanasema, historia ni mwalimu mzuri sana. Mwaka huu nimesoma vitabu vifuatavyo kuhusiana na Rwanda:

38. Behind The Presidential Curtain — Noble Marara

39. The Rwanda Crisis: History of a Genocide — Gerard Prunier

40. A Thousand Hill — Stephen Kinzer

41. Shake Hands With The Devil — Romeo Dallaire

42. Left to Tell — Immaculee Ilibagiza

43. Stepp’d in Blood — Andrew Wallis

44. Silent Accomplice: The Untold Story of France’s Role in Rwandan Genocide — Andrew Wallis

45. Conspiracy to Murder: The Rwandan Genocide — Linda Melvern

46. As We Forgive: Stories of Reconciliation from Rwanda — Catherine Claire Larson

47. Media and Mass Atrocity: The Rwanda Genocide and Beyond — Allan Thompson (Ed.)

VITABU VYA USHAIRI

Kama mshairi, miongoni mwa vitabu ninavyopenda kuvisoma mara kwa mara, ni vitabu vya ushairi. Wanasema, ushairi ni mawazo makubwa kwenye ujazo mdogo. Kwa mwaka huu wa 2019, nimesoma vitabu kadhaa vya ushairi. Ajabu, vyote vi katika Kiswahili.

48. Mwanangu Rudi Nyumbani — Dotto Rangimoto

49. Karibu Ndani — Euphras Kezilahabi

50. Mapenzi Bora — Shaaban Robert

51. Machozi Yameniishiya — Mohammed Ghassani

52. Mashairi ya Chekacheka — Theobald Mvungi

53. Teuzi za Nafsi — Francis Semghanga

KUHUSU KUANDIKA

Mwaka huu, nimeandika kazi nne. Zote hazijachapwa bado. Pengine, mwanzoni mwa mwaka ujao.

1.Rafu — riwaya ya Kiswahili. Kisa kinachomhusu Lina, mwanamke aliyeondokewa na mume wake katika mazingira ya kutatanisha. Mume alikwenda kutazama mpira. Hakurudi nyumbani. Baadaye, Lina anapoambiwa kuwa mumewe alikufa baada ya kushikwa ghafla na kiharusi, hakubaliani na maelezo hayo. Anaamua kuusaka ukweli kwa mbinu anazozijua yeye mwenyewe.

2. Mioyo Miongoni Mwetu — Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya kitabu cha Hearts Among Ourselves kilichoandikwa na dada na rafiki yangu Mnyarwanda Assumpta Happy Umwagarwa. Dada Happy alinibarikia fursa ya kukiandika kitabu chake kinachosisimua sana katika Kiswahili. Humo, kuna msichana Karabo, aliyezama katika mapenzi na Shema, huku akipendwa sana na Sugira; lakini, akiteswa na chuki za Kihutu-Kitusi baada ya mauaji ya kimbari.

3. Wasifu wa Mwanamuziki — Kimsingi, hili si jina la kitabu. Jina la kitabu na la mwanamuziki huyu wa Bongo Fleva vitafahamika hapo baadaye kidogo. Kwa ufupi, nimeandika wasifu wa mwanamuziki huyu fundi wa kuandika mashairi katika nyimbo zake. Pamoja na kuwa na muda mfupi kwenye tasnia, ukilinganisha na wengi, bado ni miongoni mwa vinara wa kuimba nyimbo zinazogusa hisia.

4. Nyonda — Kama kawaida, mimi huwa sijihesabu mwandishi kama sijaandika mashairi. Hivyo, mwaka huu, pamoja na kutingwa na pilika za huku na kule, nimeandikaandika mashairi. Nyonda ni mkusanyiko wa mashairi yanayoyagusa maisha yetu ya kila siku lakini yakiwa yamesimuliwa kwa mtindo wa mapenzi.

KUHUSU KUHARIRI

Kama inavyosema orodha juu kabisa, kwa mwaka huu nimehariri miswada minne ya waandishi wenzangu wa Kitanzania. Kuhariri ni jambo la kipekee sana. Inakufanya usome kazi ya mtu kwa jicho la tatu. Ufanye tafiti. Uulizane na watu wawili watatu. Huwa nasema, bora kuandika, kuliko kuhariri. Hata hivyo, nawashukuru sana walioniamini kuyapitisha macho yangu kwenye kazi zao. Ilikuwa heshima kubwa sana kwangu.

Panapo majaliwa, mwakani natarajia kusoma zaidi na kuandika zaidi.

Nakutakieni mwisho mwema wa 2019, pia, heri na fanaka kwa mwaka 2020.

Fadhy Mtanga,

Mbeya, Tanzania.

Jumamosi, Disemba 28, 2019.

--

--

Fadhy Mtanga
Fadhy Mtanga

Written by Fadhy Mtanga

Umfundisi | Author | Creative Writer | Biographer | Editor | Photographer | Painter | Translator | Social Scientist | Hodophile | Chef

No responses yet