SHAIRI: Uliniambia
Apr 19, 2024
Ndiyo,
Uliniambia ningoje,
Ndiyo ninangoja,
Ila hukuniambia,
Ningoje hadi lini!
Ndiyo,
Ninangoja,
Si uliniambia,
Ningoje?
Ninangoja,
Ndiyo ninangoja,
Nitangoja,
Leo na kesho,
Kesho na keshokutwa,
Mtondo na mtondogoo.
Uliniambia,
Hubarikiwa wenye kusubiri,
Mimi ni nani,
Nisizitake baraka,
Ulizoniambia?
Ndiyo, ninangoja,
Singoji kwinginewe,
Ninakungoja wewe;
Niambie basi,
Ningoje hadi lini?
©Fadhy Mtanga, 2024