Member-only story

Safari ya Victoria Falls

Fadhy Mtanga
14 min readSep 13, 2023

--

MAHALI FULANI BARANI Afrika, takribani kilometa 1,600 kutoka katikati ya jiji la Mbeya, nchi ya Zambia inakutana na Zimbabwe. Makutano hayo yanaporomosha maji ya mto Zambezi kwenye gema pana, na maji hayo yanapomwagika chini yanatoa mvuke unaolitisika anga. Watu wa kabila la Tonga (wanaopatikana Kusini mwa Zambia na Kaskazini ya Zimbabwe) wanauita Mosi-oa-Tonya, kwamba, moshi unaounguruma.

Moshi Unaounguruma

Huu ni mwongozo wa namna gani unaweza kuyazuru maporomoko hayo ya kipekee zaidi ulimwenguni. Maelekezo yangu ni endapo utatokea Mbeya mjini kwa kutumia usafiri wa umma (basi) ama kuendesha gari binafsi.

Gharama nitazoziweka ni kwa dola za Kimarekani ili kupata gharama halisi wakati wowote unapotaka kusafiri. Kumbuka, thamani ya dola ipo imara ukilinganisha na shilingi ya Tanzania, kwacha ya Zambia ama dola ya Zimbabwe.

Maelezo haya yatokana na uzoefu binafsi katika safari zangu.

Siku ya kwanza

Kama unatumia usafiri wa umma ama gari binafsi, ninashauri uondoke Mbeya mchana na kupanga kulala Tunduma/Nakonde.

Unachokifanya, siku hiyo ukiwasili Tunduma, ni kwenda moja kwa moja One Stop Border Post (OSBP) upande wa Nakonde. Hutotumia upande wa Tunduma. Ukiwasili OSBP upande wa Nakonde utagonga muhuri kwenye dirisha la Uhamiaji Tanzania kuondoka nchini na hatua moja tu dirisha la pembeni…

--

--

Fadhy Mtanga
Fadhy Mtanga

Written by Fadhy Mtanga

Umfundisi | Author | Creative Writer | Biographer | Editor | Photographer | Painter | Translator | Social Scientist | Hodophile | Chef

No responses yet