Fadhy Mtanga
Jan 25, 2022

--

Euphrase Kezilahabi ni fundi wa falsafa ya maisha. Kazi zake zilizojikita katika existentialism zinaakisi hasa maisha.

Watu wengi husema hawamwelewi marehemu Prof. Kezilahabi hususani wanapomsoma katika Nagona na Mzingile.

Prof Kezilahabi ameyatazama maisha katika namna ya kipekee sana. Anatoa majibu ya maswali mengi kuhusiana na falsafa ya maisha.

Baada ya kumsoma kwenye Rosa Mistika, tafadhali msome kwenye Kichwa Maji, Dunia Uwanja wa Fujo, Nagona na Mzingile na pia pasi kukosa diwani yake ya Karibu Ndani.

Kwenye kazi yangu ya Rafu, nilitumia Rosa Mistika kufumbua mafumbo fulani.

Ahsante sana kutushirikisha kazi hii mufti.

--

--

Fadhy Mtanga
Fadhy Mtanga

Written by Fadhy Mtanga

Umfundisi | Author | Creative Writer | Biographer | Editor | Photographer | Painter | Translator | Social Scientist | Hodophile | Chef

Responses (1)